Cybercrimes Act __________________________________________________________________ kinyume na sheria. (2) Waziri anaweza kuweka masharti kuhusiana na utaratibu wa watoa huduma kwa jili ya(a) kutoa taarifa kwa mamlaka husika ya umma kuhusiana na shughuli zilizo kinyume na sheria zinazofanywa au taarifa inayotolewa na watumiaji wa huduma zao; (b) kuzipatia mamlaka husika taarifa zitakazowezesha kuwatambua watumia huduma, baada ya maombi. (3) Mtoa huduma hatawajibika kwa uwekaji wazi wa data iliyotolewa kihalali kwa mtu wa tatu baada ya kuthibitisha kwamba: (a) mtu huyo wa tatu alitenda hivyo pasipo mtoa huduma ya mtandao kufahamu; au (b) mtoa huduma alitekeleza wajibu unaostahili na alitumia ujuzi ili kuzuia uwekwaji wazi wa data hizo. (4) Pale ambapo mtoa huduma atakuwa na uelewa juu ya taarifa au kitendo cha kihalifu kwenye mfumo wa kompyuta ambao upo chini ya udhibiti wake, atatakiwa(a) kuondoa taarifa juu ya kitendo hicho; (b) kusimamisha au kusitisha huduma; (c) kutaarifu mamlaka husika juu ya kitendo au taarifa hiyo, maelezo na utambuzi wa muhusika anayepewa huduma. Mtoa huduma ya kuingia kwenye mfumo 40.-(1) Mtoa huduma ya uwezo wa kuingia kwenye mfumo hatawajibika kwa kurusha au kuendesha mfumo wa kompyuta kwa ajili ya mtu mwingine ikiwa yeye ni mtoa huduma tu ya kuwezesha kuingia kwenye mfumo wa kompyuta au kuendesha vifaa kupitia mfumo wa kompyuta ulio chini ya mamlaka yake kwa masharti kwamba mtoa huduma: (a) haanzishi urushaji mawasiliano; (b) hachagui mpokeaji wa mawasiliano; au (c) hachagui au habadilishi data iliyoko kwenye mawasiliano. (2) Mawasiliano na masharti ya uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa kompyuta yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) yatajumuisha, utunzaji wa taarifa iliyosambazwa kwa madhumuni ya kuendeleza mawasiliano kwenye mfumo wa kompyuta kwa njia inayojiendesha yenyewe kwa kupitia mtu kati na kwa muda kwa kuzingatia kwamba mawasiliano yanafanyika kwa(a) madhumuni ya kuendesha na kusambaza taarifa katika mfumo wa 48

Select target paragraph3