Cybercrimes Act __________________________________________________________________ (c) maelezo ya hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa, madhumuni, kiasi na muda wa matumizi unaokusudiwa. (3) Afisa utekelezaji wa sheria atahakikisha kuwa mabadiliko yaliyofanywa kwenye mfumo wa kompyuta au data iliyomo kwenye kompyuta kuhusiana na mtuhumiwa zinajikita kwenye marekebisho yaliyo ya msingi kwa ajili ya uchunguzi na kwamba mabadiliko yanafanywa baada ya kukamilika kwa uchunguzi. (4) Wakati wa uchunguzi, afisa utekelezaji wa sheria ataingiza: (a) mbinu za kiufundi zilizotuimika, muda na terehe ya maombi; (b) utambuzi wa mfumo wa kompyuta na maelezo ya mabadiliko yaliyofanyika wakati wa uchunguzi; (c) taarifa yoyote iliyopatikana; (5) Taarifa iliyopatikana italindwa dhidi ya mabadiliko, kufutwa bila ya idhini na kuigia kwenye mfumo bila idhini. (6) Idhini iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa halali kwa kipindi cha siku kumi na nne. (7) Mahakama inaweza, kufuatia maombi, kuongeza muda uliotolewa chini ya kifungu kidogo cha (6) kwa kipindi kingine cha siku kumi na nne au kwa kipindi kingine kwa kadri itakavyoona inafaa. (8) Iwapo mchakato wa uwekaji wa kifaa unahitaji kutembelea eneo, masharti ya kifungu cha 30 yatatumika. (9) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), mahakama inaweza, kufuatia maombi, kumuamuru mtoa huduma awezeshe mchakato wa kuweka kifaa. (10) Waziri anaweza, kwa Taarifa itakayochapishwa kwenye Gazeti la Serikali, kuainisha makosa chini ya Sheria hii ambayo mahakama inaweza kutoa amri ya kutumia kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi. Usikilizaji wa maombi 38. Utaratibu wa kusikiliza maombi chini ya Sehemu hii utafanywa kwa upande mmoja na kwa siri. SEHEMU YA TANO WAJIBU WA MTOA HUDUMA Kutowajibika kufanya ufuatiliaji 39.-(1) Wakati wa kutoa huduma chini ya Sehemu hii, mtoa huduma(a) hata wajibika kufuatilia data ambayo anaisambaza au kuhifadhi; (b) tafuta maelezo au mazingira yanayoashiria shughuli zinazofanywa 47

Select target paragraph3