Cybercrimes Act __________________________________________________________________ kompyuta; (b) namna ambayo kwa kawaida haiwezi kupatikana isipokuwa tu kwa mpokeaji mlengwa; (c) muda ambao sio mrefu sana zaidi ya muda unaofaa kuuwasilisha ujumbe husika kwa mlengwa. Mtunza Data 41.-(1) Mtunza Data hatawajibika kuhusiana na taarifa zilizohifadhiwa kwa maombi ya mtumiaji wa huduma hiyo, kwa masharti kwamba(a) anaondoa au kusitisha upatikanaji wa taarifa baada ya kupokea amri kutoka taasisi yenye mamlaka au mahakama ya kuondoa taarifa zilizo kinyume cha sheria; (b) baada ya kufahamu kuwa taarifa iliyohifadhiwa iko kinyume cha sheria ataitaarifu mara moja taasisi husika. (2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika pale ambapo mpokeaji anafanya hivyo chini ya mamlaka ya mtoa huduma. Mhifadhi data kwa muda mfupi 42. Mtoa huduma ya kuhifadhi data hatawajibika kwa ajili ya utunzaji wa taarifa ikiwa(a) habadilishi taarifa; (b) anatekeleza masharti ya utoaji wa uwezo wa kuingia kwenye mfumo; (c) anatekeleza kanuni kuhusiana na uboreshaji wa taarifa zilizoainishwa katika namna inayotambulika na walio wengi na kutumika kwenye soko; (d) haiingiliani na matumizi halali ya teknolojia inayotambulika na wengi na ianyotumika sokoni kwa ajili ya data kwa ajili ya matumizi ya taarifa hiyo; na (e) anachukua hatua za haraka kuondoa au kusitisha matumizi ya/kufikiwa kwa taarifa ambayo imetunzwa baada ya kupokea taarifa kamili kwamba taarifa iliyo kwenye chanzo cha mawasiliano imeondolewa kutoka kwenye mtandao au ufikiwaji wake umesitishwa/ matumizi yake yamesitishwa au kwamba mahakama au mamlaka husika imeamuru itolewe au isitishwe. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti 43. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti hatawajibika kwa taarifa aliyounganisha iwapo(a) haraka iwezekanavyo anaondoa au anasitisha matumizi ya taarifa baada ya kupokea amri kutoka kwa mamlaka husika ya kuondoa kiunganishi hicho; na 49

Select target paragraph3