Cybercrimes Act __________________________________________________________________ (b) baada ya kupata uelewa kuhusiana na taarifa zilizo kinyume na sheria kwa namna nyingine zaidi ya amri ya mamlaka ya umma, haraka iwezekanavyo ataitaarifu mamlaka husika. Mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa Notisi ya kuondoa 44.-(1) Mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa hatawajibika kwa matokeo ya utafutaji huo, kwa masharti kwamba(a) haanzishi mawasiliano; (b) hachagui mpokeaji wa mwasiliano; na (c) hachagui au kubadilisha taarifa iliyoko kwenye mawasiliano. (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “mtoa huduma ya utafutaji wa taarifa” maana yake ni mtu anayetengeneza au anayeendesha huduma ambayo inatafuta taarifa inayotengeneza kiashiria inayohusiana na taarifa za mtandao au anawezesha upatikanaji wa vifaa vya kielektroniki kwa ajili ya utafutaji wa taarifa inayotolewa na mtu mwingine. 45.-(1) Mtu anaweza, kupitia notisi ya kuondoa kumtaarifu mtoa huduma(a) kuhusiana na data au taarifa iliyomnyima mpokeaji au mtu wa tatu haki ya huduma; (b) vitu au shughuli ambayo ni kinyume cha sheria; au (c) suala lolote linalotekelezwa au linalotolewa kinyume cha sheria hii au sheria nyingine. (2) Kwa madhumuni ya sehemu hii, notisi ya kuondoa itakuwa katika hali ya kudumu ikitumwa na mlalamikaji kwenda kwa mtoa huduma au wakala wake na itajumuisha(a) jina kamili na anuani ya mlalamikaji; (b) saini ya mlalamikaji; (c) maelezo ya haki inayodaiwa kuvunjwa; (d) maelezo juu ya shughuli ambayo inadaiwa kuwa chimbuko la kitendo kilicho kinyume cha sheria; (e) hatua ya utatuzi inayotakiwa kuchukuliwa na mtoa huduma kuhusiana na lalamiko; (f) maelezo kuwa mlalamikaji anatenda kwa nia njema; (g) maelezo ya mlalamikaji kuwa, kwa ufahamu wake, taarifa iliyomo kwenye taarifa zilizochukuliwa ni sahihi. (3) Mtu anayewasilisha taarifa kwa mtoa huduma kuhusiana na muamala usio 50

Select target paragraph3