Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
kinyume na sheria.
(2) Waziri anaweza kuweka masharti kuhusiana na utaratibu wa watoa
huduma kwa jili ya(a) kutoa taarifa kwa mamlaka husika ya umma kuhusiana na shughuli zilizo
kinyume na sheria zinazofanywa au taarifa inayotolewa na watumiaji wa
huduma zao;
(b) kuzipatia mamlaka husika taarifa zitakazowezesha kuwatambua watumia
huduma, baada ya maombi.
(3) Mtoa huduma hatawajibika kwa uwekaji wazi wa data iliyotolewa kihalali
kwa mtu wa tatu baada ya kuthibitisha kwamba:
(a) mtu huyo wa tatu alitenda hivyo pasipo mtoa huduma ya mtandao
kufahamu; au
(b) mtoa huduma alitekeleza wajibu unaostahili na alitumia ujuzi ili kuzuia
uwekwaji wazi wa data hizo.
(4) Pale ambapo mtoa huduma atakuwa na uelewa juu ya taarifa au kitendo
cha kihalifu kwenye mfumo wa kompyuta ambao upo chini ya udhibiti wake,
atatakiwa(a) kuondoa taarifa juu ya kitendo hicho;
(b) kusimamisha au kusitisha huduma;
(c) kutaarifu mamlaka husika juu ya kitendo au taarifa hiyo, maelezo na
utambuzi wa muhusika anayepewa huduma.
Mtoa huduma
ya kuingia
kwenye mfumo
40.-(1) Mtoa huduma ya uwezo wa kuingia kwenye mfumo hatawajibika kwa
kurusha au kuendesha mfumo wa kompyuta kwa ajili ya mtu mwingine ikiwa yeye ni
mtoa huduma tu ya kuwezesha kuingia kwenye mfumo wa kompyuta au kuendesha
vifaa kupitia mfumo wa kompyuta ulio chini ya mamlaka yake kwa masharti kwamba
mtoa huduma:
(a) haanzishi urushaji mawasiliano;
(b) hachagui mpokeaji wa mawasiliano; au
(c) hachagui au habadilishi data iliyoko kwenye mawasiliano.
(2) Mawasiliano na masharti ya uwezo wa kuingia kwenye mfumo wa
kompyuta yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) yatajumuisha, utunzaji wa
taarifa iliyosambazwa kwa madhumuni ya kuendeleza mawasiliano kwenye mfumo
wa kompyuta kwa njia inayojiendesha yenyewe kwa kupitia mtu kati na kwa muda
kwa kuzingatia kwamba mawasiliano yanafanyika kwa(a) madhumuni ya kuendesha na kusambaza taarifa katika mfumo wa
48