Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
au kutumikia kifungo alichohukumiwa kutumikia.
(4) Bila kujali kifungu kidogo cha (3), mahakama inaweza, kufuatia
kuwasilishwa kwa maombi na kwa sababu za msingi, kutoa amri ya kuachiliwa kwa
hati za kusafiria za mshitakiwa.
Makosa
yanayofanywa
na kampuni
49.-(1) Iwapo kampuni inatiwa hatiani kwa kosa chini ya Sheria hii, mtu
yeyote ambaye wakati wa utendaji wa kosa(a) alikuwa ni Mkurugenzi, afisa au vinginevyo anahusika na mambo ya
utawala wa kampuni hiyo;
(b) huku akiwa anajua, aliruhusu kitendo kilichopelekea kosa hilo,
atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo na anaweza kushitakiwa na kuadhibiwa
ipasavyo.
Kufifilisha
kosa
50.-(1) Bila kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi
wa Mashtaka, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa
kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na
kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha
faini kwa kosa hilo.
(2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa (a) ya maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa
na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa
lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1);
(b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na
(c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu.
Mamlaka ya
kutengeneza
Kanuni
51. Waziri anaweza kutunga Kanuni kuhusiana na jambo lolote ambalo
linatakiwa kuainishwa na Sheria hii au ambalo ni la umuhimu au uharaka kwa ajili ya
utekelezaji wa masharti ya Sheria hii.
_______________
MADHUMUNI NA SABABU
______________
52