Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
halali, huku akijua kuwa taarifa hiyo ni potofu, atakuwa ametenda kosa na akitiwa
hatiani, atatakiwa kulipa faini ya shilingi million tano au kifungo cha mwaka mmoja
au vyote.
(4) Mtoa huduma hatawajibika kwa kuondoa taarifa ikiwa ameifanya kwa
mujibu wa sheria hii.
Wajibu
mwingine
kutoadhiriwa
na sheria
46. Sehemu hii haitaathiri wajibu wa mtoa huduma:
(a) uliotolewa na makubaliano;
(b) ambaye anatenda kwa namna hiyo chini ya kibali au mfumo wa usimamizi
uliotajwa chini ya sheria yoyote;
(c) uliotolewa na sheria au amri ya mahakama ili kutoa, kuzuia au kukataza
uingiwaji kwenye mawasiliano ya kieletroniki au kusitisha au kuzuia
kitendo kisicho cha halali.
SEHEMU YA SITA
MASHARTI YA JUMLA
Kinga
47.-(1) Bila kujali sheria nyingine yoyote kinyume na haya, jambo au kitu
chochote kitakachofanywa na afisa utekelezaji wa sheria, katika utekelezaji wa
majukumu yake chini ya Sheria hii, hakitampelekea afisa utekelezaji wa sheria
kuwajibika moja kwa moja.
(2) Mtu hatawajibika kuhusiana na utekelezaji wa kitendo chochote au
kutokutenda, iwapo kitendo hicho au kutokutenda huko kulifanywa kwa nia njema na
siyo kwa uzembe, kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii.
Utaifishaji
mali
48.-(1) Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya Sheria hii, mahakama inaweza
kutoa amri kwa ajili ya utaifishaji wa(a) mali yoyote inayoonekana kuwa ni sehemu ya mapato yatokanayo na kosa;
na
(b) chombo chochote au mali iliyotumika au inayokusudiwa kutumika
kutenda au kufanikisha utendaji wa kosa.
(2) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), mahakama
inaweza kumuamuru mtu aliyetiwa hatiani kumlipa fidia mtu aliyeathirika na kosa
hilo kwa kadri ambavyo mahakama itaona inafaa.
(3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa lililofanywa chini ya Sheria hii
atawasilisha hati yake ya kusafiria kwa mamlaka husika hadi hapo atakapolipa faini
51