Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
Madhumuni ya Muswada huu ni kutunga sheria ambayo itaainisha makosa
yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi
wa kielektroniki.
Muswada unaopendekezwa umegawanyika katika Sehemu Saba.
Sehemu ya Kwanza, inaainisha masharti ya awali, ikiwa ni pamoja na jina
la Sheria, tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria na tafsiri ya maneno mbalimbali
yaliyotumika katika Muswada huu.
Sehemu ya Pili, inaainisha makosa na adhabu dhidi ya makosa hayo ndani
ya sheria hii.
Sehemu ya Tatu, inatoa mamlaka ya mahakama katika kusikiliza na
kuamua mashauri yanayohusu makosa ya uhalifu wa mtandao yaliyoainishwa
katika sheria inayopendekezwa.
Sehemu ya Nne, inaainisha utaratibu juu ya upekuzi na ukamataji wa vifaa
vyenye taarifa zinazohitajika kwa ajili ya upelelezi.
Sehemu ya Tano, inaainisha wajibu wa watoa huduma za mtandao wakati
wa kutoa huduma hizo.
Sehemu ya Sita, inaweka masharti ya jumla ikiwa ni pamoja na kinga kwa
maafisa utekelezaji wa sheria, utaifishaji wa mali zinazohusiana na makosa ya
mtandao, ufifilishaji wa makosa na uwajibikaji kwa makosa yanayofanywa na
kampuni.
53