Cybercrimes Act __________________________________________________________________ uongo maandishi, alama au aina nyingine yoyote kwenye mfumo wa kompyuta, endapo taarifa, data, au maelezo hayo ni ya uongo, yanapotosha au yasiyo sahihi, atakuwa ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia adhabu ya kifungo kisichopungua miezi sita au vyote. Ubaguzi 17.-(1) Mtu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta(a) hatazalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya kuvisambaza; (b) hatatoa au kuwezesha kupatikana vitu vya kibaguzi ; au (c) hatarusha vitu vya kibaguzi. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Matusi ya kibaguzi 18.-(1) Mtu hatamdhihaki mtu mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta, kutokana na sababu kuwa mtu huyo mwingine ni mmoja kati ya kundi linalotambulika kwa tabaka, rangi, asili, utaifa, kabila au dini fulani. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Mauaji ya kimbari 19.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa vitu vinavyochochea, kanusha, punguza au halalisha matendo yanayopelekea mauaji ya kimbari na makosa dhidi ya binadamu kwa kupitia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni kumi au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua miaka mitatu au vyote. Taarifa zinazotumwa bila ridhaa 20.-(1) Mtu(a) hataanzisha usambazaji wa taarifa zinazotumwa bila ridhaa; (b) hatarusha tena au kusambaza upya taarifa zinazotumwa bila ridhaa; (c) hataghushi taarifa za utambulisho na kuzituma bila ridhaa (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja 40

Select target paragraph3