Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
miaka saba au vyote.
Ponografia za
watoto
13.-(1) Mtu yeyote(a) hatachapisha ponografia za watoto kwa kupitia mfumo wa kompyuta; au
(b) hatawezesha upatikanaji au kuoneshwa kwa ponografia za mtoto kwa
kupitia mfumo wa kompyuta.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango
kisichopungua shilingi milioni hamsini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana
kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au
vyote.
(3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa chini ya kifungu hiki, pamoja na adhabu
nyingine yoyote, anaweza kuamriwa kumlipa fidia mtu ambaye ameathirika na kosa
hilo.
Ponografia
14.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa kwa kupitia katika
mfumo wa kompyuta(a) ponografia; au
(b) ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika, iwapo ni uchapishaji kuhusiana na(a) ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au kutumikia
kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote; au
(b) ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa faini isiyopungua shilingi
milioni thelathini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka
kumi au vyote.
Makosa
yanayohusiana
na utambuzi
15.-(1) Mtu hatajifanya kuwa mtu mwingine kwa kutumia mfumo wa
kompyuta.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango
kisichopungua shilingi milioni tano au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana
kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au
vyote.
Kutoa taarifa za
16. Mtu yeyote anayetoa taarifa, data au maelezo kwa njia ya picha,
39