Cybercrimes Act __________________________________________________________________ au vyote. (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “taarifa zinazotumwa bila ridhaa” maana yake ni taarifa au data za kielektroniki amabazo hazijaombwa na mpokeaji. Kufichua taarifa za upelelezi 21.-(1) Mtoa huduma anayepokea amri kuhusiana na upelelezi wa kijinai, inayohitaji usiri, hatatoa taarifa yoyote iliyopo kwenye amri hiyo isivyo halali na makusudi. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote. Kuzuia upelelezi 22. Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria ataharibu, atafuta, ataondoa, ataficha, atabadilisha au ataifanya data kompyuta kukosa maana kwa lengo la kuharibu ushahidi au kuchelewesha upelelezi atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiwango kisichopungua milioni tatu au kutumikia kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja au vyote. (2) Mtu ambaye kwa makusudi atazuia utekeleza au atashindwa kutekeleza amri iliyotolewa na sheria hii, atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Unyanyasaji kwa kupitia mtandao 23.-(1) Mtu hataanzisha au kukadimisha mawasiliano yoyote ya kielektroniki kwenda kwa mtu yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la kurubuni, kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi ya hisia. (2) Mtu akataye kiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Ukiukaji wa haki bunifu 24.-(1) Mtu hatatumia mfumo wa kompyuta kwa lengo la kukiuka haki bunifu zinazolindwa na Sheria nyingine yoyote. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika iwapo ukiukaji (a) hauhusiani na masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote; (b) unagusa masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni 41

Select target paragraph3