Cybercrimes Act __________________________________________________________________ Madhumuni ya Muswada huu ni kutunga sheria ambayo itaainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki. Muswada unaopendekezwa umegawanyika katika Sehemu Saba. Sehemu ya Kwanza, inaainisha masharti ya awali, ikiwa ni pamoja na jina la Sheria, tarehe ya kuanza kutumika kwa Sheria na tafsiri ya maneno mbalimbali yaliyotumika katika Muswada huu. Sehemu ya Pili, inaainisha makosa na adhabu dhidi ya makosa hayo ndani ya sheria hii. Sehemu ya Tatu, inatoa mamlaka ya mahakama katika kusikiliza na kuamua mashauri yanayohusu makosa ya uhalifu wa mtandao yaliyoainishwa katika sheria inayopendekezwa. Sehemu ya Nne, inaainisha utaratibu juu ya upekuzi na ukamataji wa vifaa vyenye taarifa zinazohitajika kwa ajili ya upelelezi. Sehemu ya Tano, inaainisha wajibu wa watoa huduma za mtandao wakati wa kutoa huduma hizo. Sehemu ya Sita, inaweka masharti ya jumla ikiwa ni pamoja na kinga kwa maafisa utekelezaji wa sheria, utaifishaji wa mali zinazohusiana na makosa ya mtandao, ufifilishaji wa makosa na uwajibikaji kwa makosa yanayofanywa na kampuni. 53

Select target paragraph3