Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
milioni moja au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au
vyote.
Ulinzi wa
miundo mbinu
muhimu ya
TEHAMA
28.-(1) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa kwenye Gazeti la
Serikali kuainisha mifumo ya kompyuta kama miundombinu muhimu.
(2) Amri iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1) inaweza kuainisha
vigezo, miongozo na taratibu kuhusiana na(a) usajili, ulinzi au utunzaji;
(b) usimamizi wa jumla;
(c) kuingia, kuhamisha na kudhibiti data;
(d) kuhakikisha uwepo wa audilifu au uhalali wa data au taarifa;
(e) njia zitakazotumika kuhifadhi au kutunza data;
(f) mipango ya kudhibiti majanga iwapo kutatokea uharibifu;
(g) namna na utaratibu wa kuendesha ukaguzi;
(h) jambo jingine lolote ambalo ni muhimu kwa ulinzi, usimamizi na udhibiti
wa data na rasimali nyingine.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, miundombinu muhimu ya TEHAMA
inajumuisha mali, vifaa, mifumo ya kompyuta au mitandao inayoshikika na
isiyoshikika ambayo ina umuhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi
kwamba kutokufanya kazi kwake kuna madhara ya kiusalama, kiuchumi na kijamii.
Uhujumu wa
miundombinu
muhimu wa
TEHAMA
29. Pale ambapo mtu anatenda kosa chini ya sheria hii au sheria nyingine
yoyote linalohusiana na miundombinu muhimu, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shillingi milioni mia moja au
mara tatu ya hasara aliyoisababisha au kifungo kisichopungua miaka mitano au vyote.
SEHEMU YA TATU
MAMLAKA YA MAHAKAMA
Mamlaka ya
mahakama
30.-(1) Mahakama zitakuwa na uwezo wa kusikiliza shauri lolote chini ya
Sheria hii pale ambapo kosa au sehemu ya kosa (a) limetendeka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
(b) limetendeka kwenye meli au ndege iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania;
(c) limetendwa na mtanzania; au
(d) limetendwa na mtanzania anayeishi nje Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
43