Cybercrimes Act __________________________________________________________________ milioni moja au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Ulinzi wa miundo mbinu muhimu ya TEHAMA 28.-(1) Waziri anaweza, kwa amri itakayochapishwa kwenye Gazeti la Serikali kuainisha mifumo ya kompyuta kama miundombinu muhimu. (2) Amri iliyorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1) inaweza kuainisha vigezo, miongozo na taratibu kuhusiana na(a) usajili, ulinzi au utunzaji; (b) usimamizi wa jumla; (c) kuingia, kuhamisha na kudhibiti data; (d) kuhakikisha uwepo wa audilifu au uhalali wa data au taarifa; (e) njia zitakazotumika kuhifadhi au kutunza data; (f) mipango ya kudhibiti majanga iwapo kutatokea uharibifu; (g) namna na utaratibu wa kuendesha ukaguzi; (h) jambo jingine lolote ambalo ni muhimu kwa ulinzi, usimamizi na udhibiti wa data na rasimali nyingine. (3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, miundombinu muhimu ya TEHAMA inajumuisha mali, vifaa, mifumo ya kompyuta au mitandao inayoshikika na isiyoshikika ambayo ina umuhimu kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kiasi kwamba kutokufanya kazi kwake kuna madhara ya kiusalama, kiuchumi na kijamii. Uhujumu wa miundombinu muhimu wa TEHAMA 29. Pale ambapo mtu anatenda kosa chini ya sheria hii au sheria nyingine yoyote linalohusiana na miundombinu muhimu, mtu huyo atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shillingi milioni mia moja au mara tatu ya hasara aliyoisababisha au kifungo kisichopungua miaka mitano au vyote. SEHEMU YA TATU MAMLAKA YA MAHAKAMA Mamlaka ya mahakama 30.-(1) Mahakama zitakuwa na uwezo wa kusikiliza shauri lolote chini ya Sheria hii pale ambapo kosa au sehemu ya kosa (a) limetendeka ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (b) limetendeka kwenye meli au ndege iliyosajiliwa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (c) limetendwa na mtanzania; au (d) limetendwa na mtanzania anayeishi nje Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 43

Select target paragraph3