Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
endapo kitendo alichokitenda mtu huyo kingekuwa ni kosa chini ya sheria ya
nchi hiyo;
(e) limetendwa na mtu yeyote, bila kujali utaifa au ukaazi wake au eneo husika,
iwapo kosa limefanyika(i) kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kifaa au data zilizoko ndani ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; au
(ii) dhidi ya mfumo wa kompyuta, kifaa au data au mtu aliye ndani ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
(2) Katika kifungu hiki, neno “mahakama” lina maana ya mahakama yenye
mamlaka.
SEHEMU YA NNE
UPEKUZI NA UKAMATAJI
Upekuzi na
ukamataji
31.-(1) Askari Polisi mkuu wa kituo au afisa utekelezaji wa sheria mwenye
cheo cha askari mkuu wa kituo, baada ya kuridhika kuwa kuna sababu za msingi
kushuku au kuamini kuwa mfumo wa kompyuta(a) unaweza kutumika kuthibitisha kosa;
(b) unachukuliwa na mtu yeyote kutokana na kosa,
kutoa hati ya upekuzi itakayo muidhinisha afisa utekelezaji wa sheria (i) kuingia kwenye eneo kwa lengo la kupekua au kukamata kifaa au
mfumo wa kompyuta;
(ii) kuiwekea ulinzi data iliyopatikana;
(iii) kuongeza wigo wa upekuzi au uwezo wa kuingia kwenye mfumo
mwingine iwapo afisa utekelezaji wa sheria anayefanya upekuzi
anazo sababu za kuaminika kuwa data inayotafutwa, inatunzwa
kwenye mfumo mwingine wa kompyuta au sehemu yake.
(2) Upekuzi chini ya kifungu hiki utafanyika kwa mujibu wa sheria zinazo
simamia masuala ya upekuzi na ukamataji wa mali.
(3) Iwapo kifaa au mfumo wa kompyuta umeondolewa au hauingiliki
kutokana na upekuzi au ukamataji wa mali, afisa utekelezaji wa sheria, wakati wa
upekuzi na ukamataji wa mali (a) ataandaa orodha ya vitu vyote vilivyokamatwa au kufanywa visiingilike,
ikijumuisha muda ambao mali ilikamatwa;
(b) atampatia nakala ya orodha ya mali iliyokamatwa mtu anayemiliki au
mwangalizi wa mfumo husika wa kompyuta.
44