Cybercrimes Act __________________________________________________________________ ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote Kifaa kisicho halali 10.-(1) Mtu hatajishughulisha au kumiliki, kinyume cha sheria(a) kifaa ikijumuisha programu ya kompyuta iliyotengenezwa au inayotumiwa kwa madhumuni ya kutenda kosa; (b) namba ya siri ya kompyuta, ishara ya kuingilia au data kama hiyo ambayo inaweza kutumika na mtu yoyote kuingilia mfumo wa kompyuta au sehemu yake kwa lengo la kutenda kosa. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni kumi au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote Kughushi kunakohusiana na masuala ya kompyuta Udanganyifu unaohusiana na kompyuta 11.-(1) Mtu hataingiza, hatabadilisha, hatachelewesha, hatasambaza au hatafuta data kompyuta iliyogushiwa kwa lengo la kutaka itumike kwa madhumuni halali, bila kujali kama taarifa hiyo inasomeka au haisomeki. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote. 12.-(1) Mtu hatasababisha kupotea kwa mali ya mtu mwingine(a) kwa kuongeza, kubadilisha, kufuta, kuchelewesha, kusambaza au kuzuia data kompyuta; au (b) kwa kuingilia utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta, kwa udanganyifu au ya uongo kwa lengo la kujipatia bila haki manufaa ya kiuchumi. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua 38

Select target paragraph3