Cybercrimes Act __________________________________________________________________ (a) anawasilisha, anafichua au anasambaza data kompyuta, programu ya kompyuta, ishara ya kuingilia au agizwa kwa mtu ambaye hajaidhinishwa; (b) anapokea data kompyuta ambayo haijaidhinishwa, ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote. (3) Mtu ambaye isivyo halali na kwa makusudi anaharibu au anabadili data yoyote ya kompyuta, iwapo data hiyo inatakiwa kutunzwa kisheria au ni ushahidi kwenye shauri lolote chini ya Sheria hii kwa(a) kuondoa au kubadilisha data, programu au taarifa nyingine yoyote iliyoko ndani au nje ya mfumo wa kompyuta; (b) anawasha, anaingiza au anapakua programu ambayo imetengenezwa kwa lengo la kuondoa au kubadilisha data, programu au aina yoyote ya taarifa ilioyoko ndani au nje ya mfumo wa kompyuta; au (c) anatengeneza, anabadilisha au anaharibu namba ya siri, namba binafsi ya utambulisho au namna inayotumika kuingika kwenye mfumo wa kompyuta, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano au vyote. Ujasusi data Sura ya 47 Kuingilia mfumo kinyume cha sheria 8.-(1) Bila kuathiri masharti ya sheria ya Usalama wa Taifa, mtu hataingilia pasipo idhini na kujipatia data kompyuta iliyokingwa dhidi ya kuingiliwa. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano au vyote 9. Mtu ambaye, kinyume cha sheria na kwa makusudi anazuia au anaingilia(a) utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta; (b) matumizi au uendeshaji wa mfumo wa kompyuta, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho 37

Select target paragraph3