Cybercrimes Act __________________________________________________________________ mtandao au chombo cha kuhifadhia data; “mtoa njia” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya usambazaji wa data za kielekroniki kwa kusambaza taarifa zilizotolewa na au kwa mtumiaji wa huduma katika mtandao wa mawasiliano au anayetoa fursa ya kuingia kwenye kompyuta au mtandao; “mhifadhi data ” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya uhifadhi wa data za kielektroniki kwa njia inayojiendesha yenyewe, kwa kupitia mtu kati au kwa utunzaji wa taarifa kwa muda mfupi kwa madhumuni ya kuwezesha upatikanaji wa taarifa kwa kwa watumiaji wengine wa huduma kiufanisi zaidi pale watakapoomba; “mtoto” maana yake ni mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na nane; “ponografia za watoto” maana yake ni aina yoyote ya picha na filamu za ngono zinazo ashiria au kumuonesha: (a) mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi katika matendo ya ngono; (b) mtu anayeonekana kama mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi katika matendo ya ngono; au (c) taswira inayoashiria mtoto akiwa anashiriki kwa udhahiri katika matendo ya ngono; “mfumo wa kompyuta” maana yake ni kifaa au mchanganyiko wa vifaa, ikijumuisha mtandao, vifaa vya kuingizia na vya kutolea na ambavyo vinaweza kutumika pamoja na majalada yaliyo na programu za kompyuta, maelezo ya kielektroniki, data za kuingizia na data za kutolea zinazotunza data za hesabu za miongo zilizo na mantiki na udhibiti wa utolewaji wa mawasiliano na majukumu mengine; “data kompyuta” maana yake ni uwasilishaji wa maelezo, dhana, taarifa au maelekezo katika namna inayofaa kwa ajili ya kuchakata katika mfumo wa kompyuta,ikijumuisha programu inayofaa kwa ajili ya kuwezesha mfumo wa kompyuta kutelekeza kazi fulani; “chombo cha utunzaji wa data ” maana yake ni kifaa chochote au kitu ambacho kutoka kwake data kompyuta au taarifa inaweza kuchakata kwenye mfumo wa kompyuta au kutengenezwa ama kwa msaada wa kifaa kingine au kitu au la; “kifaa” inajumuisha: (a) programu ya kompyuta, namba tambuzi, mianzi laini au application; 33

Select target paragraph3