Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
_____
TAARIFA
_____
Muswada huu utakaowasilishwa Bungeni umechapishwa pamoja na madhumuni na
sababu zake kwa ajili ya kutoa taarifa ya jumla kwa umma.
Dar es Salaam,
3 Februari, 2015
OMBENI Y. SEFUE
Katibu wa Baraza la Mawaziri
MUSWADA
wa
Sheria inayoainisha makosa yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa
kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, kuweka utaratibu
wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi ya ushahidi wa kielektroniki na
masuala mengine yanayohusiana na hayo.
IMETUNGWA na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
SEHEMU YA KWANZA
MASHARTI YA AWALI
Jina na tarehe
ya kuanza
kutumika
1. Sheria hii itaitwa Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015. Sheria hii
itaanza kutumika tarehe ambayo Waziri ataiteua na kuitangaza katika Gazeti la
Serikali.
Matumizi
2. Isipokuwa kwa kifungu cha 50, Sheria hii itatumika Tanzania Bara na
Tanzania Zanzibar.
Tafsiri
3. Katika sheria hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo“kuingia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta maana yake ni kuingia, kutoa maelekezo,
kuwasiliana, kuhifadhi data au kupokea data kutoka katika mfumo wa
kompyuta au vinginevyo kutumia rasilimali zozote za mfumo wa kompyuta au
32