Cybercrimes Act __________________________________________________________________ (4) Mtu anayemiliki au mwangalizi wa mfumo wa kompyuta anaweza kumuomba afisa utekelezaji wa sheria ruhusa ya kuingia au kudurufu taarifa zilizopo kwenye mfumo wa kompyuta baada ya ukamataji wa mali. (5) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (4), afisa utekelezaji wa sheria anaweza kukataa kuruhusu kuingia kwenye mfumo au kudurufu taarifa iwapo anazo sababu za msingi za kuamini kuwa kuruhusu kuingia au kudurufu taarifa(a) itakuwa ni kosa; au (b) kutaathiri(i) uchunguzi unaohusiana na upekuzi (ii) upelelezi mwingine unaoendelea; au (iii) shauri lolote lililopo mahakamani au ambalo linaweza kufunguliwa kuhusiana na uchunguzi huo. (6) Katika kifungu hiki “eneo” inajumuisha ardhi, majengo au chombo cha usafiri. Utoaji data 32.-(1) Pale ambapo data inanitajika kuwekwa wazi kwa madhumuni ya uchunguzi wa kijinai au kuendeshwa kwa kesi mahakamani, Askari Polisi Mkuu wa kituo au afisa mtekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo anaweza kutoa amri kumtaka(a) mtu yeyote kuwasilisha data iliyoainishwa ambayo mtu huyo anaimiliki au iliyo chini ya uangalizi wake ambayo imehifadhaiwa kwenye mfumo wa kompyuta; au (b) mtoa huduma yeyote, kuwasilisha taarifa kuhusiana na mteja zilizo kwenye umiliki au uangalizi wake. (2) Iwapo kitu chochote kinachohusiana na upelelezi kinajumuisha data iliyohifadhiwa kwenye mfumo wa kompyuta au kwenye kifaa, amri itachukuliwa kumtaka mtu kutoa au kuruhusu upatikanaji wa data hiyo katika namna ambayo inasomeka na inayoweza kuondolewa. Utunzaji data wa dharura 33. Pale ambapo Askari Polisi Mkuu wa kituo au afisa utekelezaji wa sheria anazo sababu za kuamini kuwa data kompyuta ambayo inahitajika kwa madhumuni ya uchunguzi inaweza kupotea au kubadilishwa, anaweza kutoa amri itakayomtaka mtu mwenye uangalizi au umiliki wa kifaa au data kompyuta kuitunza kwa kipindi kisichozidi siku kumi na nne. Utoaji na 34.-(1) Pale Askari Polisi Mkuu wa kituo au afisa mtekelezaji wa sheria 45

Select target paragraph3