Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
(b) sehemu ya mfumo wa kompyuta kama vile grafiki kadi, kadi ya kutunza
kumbukumbu, chipu au kichakataji;
(c) kifaa cha kutunzia kumbukumbu za kompyuta; na
(d) kifaa cha kuingizia na kutolea taarifa katika kompyuta na mifumo ya
kompyuta;
“mawasiliano ya kielektroniki” maana yake ni uhamishaji wa alama, ishara au data
kompyuta ya aina yoyote ile iliyotumwa yote au sehemu kwa njia ya waya,
redio, elektromagnetiki, picha ya kielektroniki, picha ya mfumo wa optika au
aina nyingine ya mfumo inayofanana na hiyo;
“ kifaa cha TEHAMA katika uchunguzi ” maana yake ni kifaa cha uchunguzi au kifaa
kinachojumuisha mianzi laini au mianzi ngumu iliyowekwa kwenye au
inayohusiana na mfumo wa kompyuta au sehemu ya mfumo wa kompyuta na
inayotumika kutekeleza kazi zinazojumuisha uingiaji kwa siri au ukusanyaji
wa taarifa za kiuchunguzi zinazohusiana na matumizi ya kompyuta au mfumo
wa kompyuta;
“zuia” kuhusiana na mfumo wa kompyuta inajumuisha(a) kusababisha kuingiliwa kielektromagnetiki kwa mfumo wa kompyuta;
(b) kuvuruga mfumo wa kompyuta kwa namna yoyote ile; au
(c) kuingiza, kutuma, kuzorotesha, kufuta, kuvuruga, kubadilisha au kuzuia
data kompyuta;
“mtunza data” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya kusambaza data kwa kutunza
taarifa inayotolewa na mtumiaji wa huduma hiyo;
“kiunganishi tovuti” maana yake ni alama, neno, msemo, sentensi, au taswira iliyo
katika tovuti au taarifa kuhusiana na chanzo kingine kinachopelekea au
kufunguka kwa tovuti nyingine;
“haki bunifu’’ maana yake ni haki zinazotokana au zinazohusiana na haki miliki, hati
bunifu, alama za biashara, na mambo mengine yanayohusiana nayo;
“kuingilia” kuhusiana na utendaji kazi wa kompyuta inajumuisha upatikanaji,
utazamaji, usikilizaji au kunukuu data yoyote ya mawasiliano ya kompyuta au
mifumo ya kompyuta kwa njia yoyote ya kielektroniki;
34