Cybercrimes Act __________________________________________________________________ “afisa utekelezaji wa sheria” maana yake ni afisa wa polisi mwenye cheo cha Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, mpelelezi, afisa Usalama wa Taifa mwendesha mashtaka au mtu aliyeidhinishwa chini ya sheria yoyote; “Waziri” maana yake ni Waziri anayehusika na masuala ya TEHAMA. “kuchapisha” maana yake ni usambazaji, uwasilishaji, uwekaji wazi, kubadilishana,uchapishaji, au usambazaji wa aina yoyote ile; “mali” maana yake ni mali ya aina yoyote, inayogusika au isiyo gusika na inajumusha: (a) fedha yoyote inayotumika au isiyotumika katika Jamhuri ya Muungano Tanzania; (b) taarifa, ikijumuisha programu, data au nakala zake, zinazoweza kusomwa na binadamu au kwa kompyuta; au (c) haki yoyote au maslahi kwenye mali; “ubaguzi” maana yake ni taarifa za namna yoyote zinazokuza au kuchochea chuki, ubaguzi au vurugu dhidi ya mtu au kundi la watu kwa msingi wa tabaka, rangi, asili,utaifa, kabila au dini; “mtoa huduma” maana yeke ni mtu au upande unaowezesha mfumo wa taarifa kupatikana kwa mtu-kati. SEHEMU YA PILI MASHARTI YANAYOHUSIANA NA MAKOSA NA ADHABU Kuingia kinyume cha sheria 4.-(1) Mtu hataingia au kusababisha kuingiliwa mfumo wa kompyuta kinyume cha sheria na kwa makusudi. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote. Matumizi ya mfumo wa kompyuta kinyume cha 5.-(1) Mtu hatatumia au kuendelea kutumia mfumo wa kompyuta, kinyume cha sheria na kwa makusudi, baada ya kuisha kwa muda ambao aliruhusiwa kutumia mfumo wa kompyuta. 35

Select target paragraph3