Cybercrimes Act __________________________________________________________________ au kutumikia kifungo alichohukumiwa kutumikia. (4) Bila kujali kifungu kidogo cha (3), mahakama inaweza, kufuatia kuwasilishwa kwa maombi na kwa sababu za msingi, kutoa amri ya kuachiliwa kwa hati za kusafiria za mshitakiwa. Makosa yanayofanywa na kampuni 49.-(1) Iwapo kampuni inatiwa hatiani kwa kosa chini ya Sheria hii, mtu yeyote ambaye wakati wa utendaji wa kosa(a) alikuwa ni Mkurugenzi, afisa au vinginevyo anahusika na mambo ya utawala wa kampuni hiyo; (b) huku akiwa anajua, aliruhusu kitendo kilichopelekea kosa hilo, atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo na anaweza kushitakiwa na kuadhibiwa ipasavyo. Kufifilisha kosa 50.-(1) Bila kuathiri sheria nyingine inayotumika Tanzania Bara, Mkurugenzi wa Mashtaka, muda wowote kabla ya mwenendo wa mahakama kuanza na kwa kuzingatia tamko la kukiri kosa kwa hiari la mshitakiwa anaweza kufifilisha kosa na kuamuru mtu huyo alipe kiasi cha pesa atakachokitaja ambacho hakitazidi kiasi cha faini kwa kosa hilo. (2) Amri ya kufifilisha kosa chini ya kifungu kidogo cha (1) itakuwa (a) ya maandishi, ikiainisha kosa lililotendeka, kiasi cha fedha zitakazolipwa na tarehe ya kufanya malipo ikiambatanisha tamko la kukubali kosa lililorejewa chini ya kifungu kidogo cha (1); (b) ni uamuzi wa mwisho na hautakatiwa rufaa; na (c) na uwezo wa kutekelezwa katika namna sawa na amri ya Mahakama Kuu. Mamlaka ya kutengeneza Kanuni 51. Waziri anaweza kutunga Kanuni kuhusiana na jambo lolote ambalo linatakiwa kuainishwa na Sheria hii au ambalo ni la umuhimu au uharaka kwa ajili ya utekelezaji wa masharti ya Sheria hii. _______________ MADHUMUNI NA SABABU ______________ 52

Select target paragraph3