Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
kompyuta;
(b) namna ambayo kwa kawaida haiwezi kupatikana isipokuwa tu kwa
mpokeaji mlengwa;
(c) muda ambao sio mrefu sana zaidi ya muda unaofaa kuuwasilisha ujumbe
husika kwa mlengwa.
Mtunza Data
41.-(1) Mtunza Data hatawajibika kuhusiana na taarifa zilizohifadhiwa kwa
maombi ya mtumiaji wa huduma hiyo, kwa masharti kwamba(a) anaondoa au kusitisha upatikanaji wa taarifa baada ya kupokea amri
kutoka taasisi yenye mamlaka au mahakama ya kuondoa taarifa zilizo
kinyume cha sheria;
(b) baada ya kufahamu kuwa taarifa iliyohifadhiwa iko kinyume cha sheria
ataitaarifu mara moja taasisi husika.
(2) Kifungu kidogo cha (1) hakitatumika pale ambapo mpokeaji anafanya
hivyo chini ya mamlaka ya mtoa huduma.
Mhifadhi data
kwa muda
mfupi
42. Mtoa huduma ya kuhifadhi data hatawajibika kwa ajili ya utunzaji wa
taarifa ikiwa(a) habadilishi taarifa;
(b) anatekeleza masharti ya utoaji wa uwezo wa kuingia kwenye mfumo;
(c) anatekeleza kanuni kuhusiana na uboreshaji wa taarifa zilizoainishwa
katika namna inayotambulika na walio wengi na kutumika kwenye soko;
(d) haiingiliani na matumizi halali ya teknolojia inayotambulika na wengi na
ianyotumika sokoni kwa ajili ya data kwa ajili ya matumizi ya taarifa hiyo;
na
(e) anachukua hatua za haraka kuondoa au kusitisha matumizi ya/kufikiwa
kwa taarifa ambayo imetunzwa baada ya kupokea taarifa kamili kwamba
taarifa iliyo kwenye chanzo cha mawasiliano imeondolewa kutoka kwenye
mtandao au ufikiwaji wake umesitishwa/ matumizi yake yamesitishwa au
kwamba mahakama au mamlaka husika imeamuru itolewe au isitishwe.
Mtoa huduma
ya
kuunganisha
tovuti
43. Mtoa huduma ya kuunganisha tovuti hatawajibika kwa taarifa
aliyounganisha iwapo(a) haraka iwezekanavyo anaondoa au anasitisha matumizi ya taarifa baada ya
kupokea amri kutoka kwa mamlaka husika ya kuondoa kiunganishi hicho;
na
49