Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
ukusanyaji wa
data nyendo
Utoaji na
ukusanyaji wa
maudhui katika
data
Amri ya
mahakama
Matumizi ya
kifaa cha
TEHAMA
katika
uchunguzi
mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo anaridhika kuwa data kompyuta inahitajika
kwa madhumuni ya uchunguzi, afisa huyo anaweza kutoa amri kwa maandishi kwa
ajili ya(a) ukusanyaji au kuweka kumbukumbu za taarifa za kompyuta zinazohusiana
na mawasilano maalum kwa kipindi maalum; au
(b) kumruhusu na kumsaidia afisa utekelezaji wa sheria kukusanya na kuweka
kumbukumbu za data hizo.
(2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki “data nyendo” maana yake ni taarifa:
(a) inayohusiana na mawasiliano kwa mfumo wa kompyuta;
(b) iliyotolewa na mfumo wa kompyuta ambao ni sehemu ya mlolongo wa
mawasiliano; na
(c) inayoonesha chanzo cha mawasiliano,njia iliyotumika, muda,ukubwa,
uelekeo na aina ya huduma zinazoambatana nazo.
35. Pale ambapo Askari Polisi Mkuu wa kituo au afisa mtekelezaji wa sheria
mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo anazo sababu za msingi za kushuku au
kuamini kuwa yaliyomo kwenye mawasiliano ya kielektroniki yanahitajika kwa
madhumuni ya uchunguzi, anaweza kutoa amri ya:
(a) kukusanya, kurekodi, kuruhusu au kuisaidia mamlaka husika kukusanya
au kurekodi taarifa zilizomo kwenye inayohusishwa na mawasiliano
maalum yaliyotolewa ka njia ya mfumo wa kompyuta; au
(b) kumuidhinisha afisa utekelezaji wa sheria kukusanya au kurekodi data kwa
kupitia njia ya kiufundi.
36. Pale ambapo utoaji data au utunzaji data wa dharura chini ya vifungu vya
31, 32, 33, 34 au 35 kwa kadri itakavyokuwa, hauwezi kufanyika bila kutumia nguvu
au kutokana na pingamizi kutoka kwa mtu mwenye kumiliki data au thamani ya
ushahidi katika data inaweza kuhifadhiwa kwa amri ya mahakama, afisa mtekelezaji
wa sheria anaweza kuomba mahakamani amri ya utoaji au utunzaji wa data.
37.-(1) Pale ambapo afisa utekelezaji wa sheria anaridhika kuwa ushahidi wa
msingi hauwezi kukusanywa kwa kutumia utaratibu uliainishwa chini ya Sehemu hii,
afisa utekelezaji huyo anaweza kuiomba mahakama kutoa amri ya kuidhinisha
matumizi ya kifaa cha uchunguzi.
(2) Maombi yaliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1) yatajumuisha(a) jina na anuani ya mtuhumiwa;
(b) maelezo ya mfumo wa kompyuta unaolengwa; na
46