Cybercrimes Act __________________________________________________________________ endapo kitendo alichokitenda mtu huyo kingekuwa ni kosa chini ya sheria ya nchi hiyo; (e) limetendwa na mtu yeyote, bila kujali utaifa au ukaazi wake au eneo husika, iwapo kosa limefanyika(i) kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kifaa au data zilizoko ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; au (ii) dhidi ya mfumo wa kompyuta, kifaa au data au mtu aliye ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2) Katika kifungu hiki, neno “mahakama” lina maana ya mahakama yenye mamlaka. SEHEMU YA NNE UPEKUZI NA UKAMATAJI Upekuzi na ukamataji 31.-(1) Askari Polisi mkuu wa kituo au afisa utekelezaji wa sheria mwenye cheo cha askari mkuu wa kituo, baada ya kuridhika kuwa kuna sababu za msingi kushuku au kuamini kuwa mfumo wa kompyuta(a) unaweza kutumika kuthibitisha kosa; (b) unachukuliwa na mtu yeyote kutokana na kosa, kutoa hati ya upekuzi itakayo muidhinisha afisa utekelezaji wa sheria (i) kuingia kwenye eneo kwa lengo la kupekua au kukamata kifaa au mfumo wa kompyuta; (ii) kuiwekea ulinzi data iliyopatikana; (iii) kuongeza wigo wa upekuzi au uwezo wa kuingia kwenye mfumo mwingine iwapo afisa utekelezaji wa sheria anayefanya upekuzi anazo sababu za kuaminika kuwa data inayotafutwa, inatunzwa kwenye mfumo mwingine wa kompyuta au sehemu yake. (2) Upekuzi chini ya kifungu hiki utafanyika kwa mujibu wa sheria zinazo simamia masuala ya upekuzi na ukamataji wa mali. (3) Iwapo kifaa au mfumo wa kompyuta umeondolewa au hauingiliki kutokana na upekuzi au ukamataji wa mali, afisa utekelezaji wa sheria, wakati wa upekuzi na ukamataji wa mali (a) ataandaa orodha ya vitu vyote vilivyokamatwa au kufanywa visiingilike, ikijumuisha muda ambao mali ilikamatwa; (b) atampatia nakala ya orodha ya mali iliyokamatwa mtu anayemiliki au mwangalizi wa mfumo husika wa kompyuta. 44

Select target paragraph3