Cybercrimes Act __________________________________________________________________ ishirini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano au vyote. Wakosaji wakuu 25.-(1) Mtu yeyote ambaye(a) anafanya kitendo au anaacha kufanya kitendo ambacho kiasi kwamba kutokutenda huko kunasababisha kutendeka kwa kosa; (b) anafanya au anaacha kufanya kitendo kwa madhumuni ya kumuwezesha au kumsaidia mtu mwingine kutenda kosa; (c) anamsaidia na kumwezesha mtu mwingine kutenda kosa; (d) anamshawishi au kumlipa mtu mwingine kufanya kosa hilo, atachukuliwa kuwa ametenda kosa na atashitakiwa kama mtu aliyetenda kosa. (2) Mtu anayemlipa mtu mwingine kufanya au kutokufanya kitendo kwa kiasi ambapo, iwapo yeye mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko, kitendo hicho kingepelekea kosa kufanyika kwa upande wake na atakuwa na hatia kwa kosa la aina hiyo na atawajibika kwa adhabu sawa kana kwamba yeye mwenyewe angefanya kitendo hicho au kutokutenda huko. Jaribio la kufanya uhalifu 26.-(1) Pale ambapo mtu anayekusudia kutenda kosa anaanza kutekeleza kusudio lake na anadhihirisha kusudio lake kwa kitendo kinachoashiria kosa, isipokuwa hatekelezi kusudio lake kwa kiasi cha kutenda kosa hilo, atachukuliwa kuwa ametenda kosa hilo. (2) Kwa madhumuni ya kifungu hiki(a) isipokuwa kwa kiasi cha adhabu haitajalisha iwapo(i) mkosaji anatenda yote ambayo ni muhimu kwa utendaji wa kosa; au (ii) utekelezaji wa kusudio lake kwa ukamilifu unazuiliwa na mazingira ambayo hayaingiliani na kusudio lake; au (iii) anaacha kutekeleza kusudio lake kwa hiari yake mwenyewe; (b) kutokana na sababu za mazingira yasiyojulikana kwa mhalifu haiwezekani kutenda kosa. (3) Mtu yeyote anayejaribu kutenda kosa chini ya sheria hii atakua ametenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita au vyote. Kula njama ya kutenda kosa 27. Mtu anayekula njama na mtu mwingine kutenda kosa chini ya Sheria hii, anatenda kosa na iwapo atatiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi 42

Select target paragraph3