Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
uongo
maandishi, alama au aina nyingine yoyote kwenye mfumo wa kompyuta, endapo
taarifa, data, au maelezo hayo ni ya uongo, yanapotosha au yasiyo sahihi, atakuwa
ametenda kosa, na akipatikana na hatia atalipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu
au kutumikia adhabu ya kifungo kisichopungua miezi sita au vyote.
Ubaguzi
17.-(1) Mtu, kwa kutumia mfumo wa kompyuta(a) hatazalisha vitu vya kibaguzi kwa madhumuni ya kuvisambaza;
(b) hatatoa au kuwezesha kupatikana vitu vya kibaguzi ; au
(c) hatarusha vitu vya kibaguzi.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua kiasi cha shilingi milioni tatu
au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Matusi ya
kibaguzi
18.-(1) Mtu hatamdhihaki mtu mwingine kwa kupitia mfumo wa kompyuta,
kutokana na sababu kuwa mtu huyo mwingine ni mmoja kati ya kundi
linalotambulika kwa tabaka, rangi, asili, utaifa, kabila au dini fulani.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Mauaji ya
kimbari
19.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa vitu vinavyochochea,
kanusha, punguza au halalisha matendo yanayopelekea mauaji ya kimbari na makosa
dhidi ya binadamu kwa kupitia mfumo wa kompyuta.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni kumi au
kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua miaka mitatu au vyote.
Taarifa
zinazotumwa
bila ridhaa
20.-(1) Mtu(a) hataanzisha usambazaji wa taarifa zinazotumwa bila ridhaa;
(b) hatarusha tena au kusambaza upya taarifa zinazotumwa bila ridhaa;
(c) hataghushi taarifa za utambulisho na kuzituma bila ridhaa
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango
kisichopungua shilingi milioni tatu au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana
kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja
40