Cybercrimes Act __________________________________________________________________ miaka saba au vyote. Ponografia za watoto 13.-(1) Mtu yeyote(a) hatachapisha ponografia za watoto kwa kupitia mfumo wa kompyuta; au (b) hatawezesha upatikanaji au kuoneshwa kwa ponografia za mtoto kwa kupitia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni hamsini au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote. (3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa chini ya kifungu hiki, pamoja na adhabu nyingine yoyote, anaweza kuamriwa kumlipa fidia mtu ambaye ameathirika na kosa hilo. Ponografia 14.-(1) Mtu hatachapisha au kusababisha kuchapishwa kwa kupitia katika mfumo wa kompyuta(a) ponografia; au (b) ponografia yoyote iliyo ya kiasherati au chafu. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika, iwapo ni uchapishaji kuhusiana na(a) ponografia, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni ishirini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote; au (b) ponografia iliyo ya kiasherati au chafu, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni thelathini au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka kumi au vyote. Makosa yanayohusiana na utambuzi 15.-(1) Mtu hatajifanya kuwa mtu mwingine kwa kutumia mfumo wa kompyuta. (2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni tano au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka saba au vyote. Kutoa taarifa za 16. Mtu yeyote anayetoa taarifa, data au maelezo kwa njia ya picha, 39

Select target paragraph3