Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni mbili au mara tatu ya
thamani ya faida iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua mwaka mmoja au vyote
Kifaa kisicho
halali
10.-(1) Mtu hatajishughulisha au kumiliki, kinyume cha sheria(a) kifaa ikijumuisha programu ya kompyuta iliyotengenezwa au inayotumiwa
kwa madhumuni ya kutenda kosa;
(b) namba ya siri ya kompyuta, ishara ya kuingilia au data kama hiyo ambayo
inaweza kutumika na mtu yoyote kuingilia mfumo wa kompyuta au
sehemu yake kwa lengo la kutenda kosa.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya
kiwango kisichopungua shilingi milioni kumi au mara tatu ya thamani ya faida
iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua
miaka mitatu au vyote
Kughushi
kunakohusiana
na masuala ya
kompyuta
Udanganyifu
unaohusiana na
kompyuta
11.-(1) Mtu hataingiza, hatabadilisha, hatachelewesha, hatasambaza au
hatafuta data kompyuta iliyogushiwa kwa lengo la kutaka itumike kwa madhumuni
halali, bila kujali kama taarifa hiyo inasomeka au haisomeki.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika, kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya
kiwango kisichopungua shilingi milioni ishirini au mara tatu ya thamani ya faida
iliyopatikana kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua
miaka saba au vyote.
12.-(1) Mtu hatasababisha kupotea kwa mali ya mtu mwingine(a) kwa kuongeza, kubadilisha, kufuta, kuchelewesha, kusambaza au kuzuia
data kompyuta; au
(b) kwa kuingilia utendaji kazi wa mfumo wa kompyuta,
kwa udanganyifu au ya uongo kwa lengo la kujipatia bila haki manufaa ya kiuchumi.

38