Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
sheria
Kuingilia
mawasiliano
kinyume cha
sheria
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho ni kikubwa kati ya kiwango
kisichopungua shilingi milioni moja au mara tatu ya thamani ya faida iliyopatikana
kinyume cha sheria, au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi sita au
vyote.
6.-(1) Mtu ambaye, kinyume cha sheria na kwa makusudi(a) anaingilia kwa kutumia njia ya kiufundi au kwa njia nyingine yoyote:
(i)
mawasilano yasiyo ya umma kwenda au kutoka au yaliyo ndani
ya mfumo wa kompyuta;
(ii)
mawasiliano yasiyo ya umma ya kieletromaniginetiki yakokayo
katika mfumo wa kompyuta usio wa umma; au
(iii) mfumo wa kompyuta usio wa umma ambao umeunganishwa na
mfumo mwingine wa kompyuta.
(b) anakwepa hatua za udhibiti zilizoelekezwa kwa ajili ya kukinga
kuingiliwa kwa maudhui yaliyomo kwenye mawasiliano yasiyo ya umma.
(2) Mtu atakayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni tano au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Kuingilia data
kinyume cha
sheria
7.-(1) Mtu ambaye, kinyume cha sheria na kwa makusudi(a) anaharibu au anazorotesha data kompyuta;
(b) anafuta data kompyuta;
(c) anabadili data kompyuta;
(d) anaifanya datamkompyuta ipoteze maana, ishindwe kutumika au ikose
ufanisi;
(e) anazuia au anaingilia matumizi halali ya data kompyuta;
(f) anazuia au anamuingilia mtu mwingine anayetumia data kompyuta
kihalali; au
(g) anamzuia mtu aliyeidhinishwa kutumia data kompyuta,
atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atawajibika kulipa faini ya kiasi ambacho
ni kikubwa kati ya kiwango kisichopungua shilingi milioni kumi au mara tatu ya
thamani ya faida iliyopatikana kinyume na sheria au kutumikia kifungo kwa kipindi
kisichopungua miaka mitatu au vyote.
(2) Mtu ambaye-
36