Cybercrimes Act __________________________________________________________________ halali, huku akijua kuwa taarifa hiyo ni potofu, atakuwa ametenda kosa na akitiwa hatiani, atatakiwa kulipa faini ya shilingi million tano au kifungo cha mwaka mmoja au vyote. (4) Mtoa huduma hatawajibika kwa kuondoa taarifa ikiwa ameifanya kwa mujibu wa sheria hii. Wajibu mwingine kutoadhiriwa na sheria 46. Sehemu hii haitaathiri wajibu wa mtoa huduma: (a) uliotolewa na makubaliano; (b) ambaye anatenda kwa namna hiyo chini ya kibali au mfumo wa usimamizi uliotajwa chini ya sheria yoyote; (c) uliotolewa na sheria au amri ya mahakama ili kutoa, kuzuia au kukataza uingiwaji kwenye mawasiliano ya kieletroniki au kusitisha au kuzuia kitendo kisicho cha halali. SEHEMU YA SITA MASHARTI YA JUMLA Kinga 47.-(1) Bila kujali sheria nyingine yoyote kinyume na haya, jambo au kitu chochote kitakachofanywa na afisa utekelezaji wa sheria, katika utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii, hakitampelekea afisa utekelezaji wa sheria kuwajibika moja kwa moja. (2) Mtu hatawajibika kuhusiana na utekelezaji wa kitendo chochote au kutokutenda, iwapo kitendo hicho au kutokutenda huko kulifanywa kwa nia njema na siyo kwa uzembe, kwa mujibu wa masharti ya Sheria hii. Utaifishaji mali 48.-(1) Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya Sheria hii, mahakama inaweza kutoa amri kwa ajili ya utaifishaji wa(a) mali yoyote inayoonekana kuwa ni sehemu ya mapato yatokanayo na kosa; na (b) chombo chochote au mali iliyotumika au inayokusudiwa kutumika kutenda au kufanikisha utendaji wa kosa. (2) Pamoja na amri iliyotolewa chini ya kifungu kidogo cha (1), mahakama inaweza kumuamuru mtu aliyetiwa hatiani kumlipa fidia mtu aliyeathirika na kosa hilo kwa kadri ambavyo mahakama itaona inafaa. (3) Mtu aliyetiwa hatiani kwa kosa lililofanywa chini ya Sheria hii atawasilisha hati yake ya kusafiria kwa mamlaka husika hadi hapo atakapolipa faini 51

Select target paragraph3