Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
au vyote.
(3) Kwa madhumuni ya kifungu hiki, “taarifa zinazotumwa bila ridhaa” maana
yake ni taarifa au data za kielektroniki amabazo hazijaombwa na mpokeaji.
Kufichua
taarifa za
upelelezi
21.-(1) Mtoa huduma anayepokea amri kuhusiana na upelelezi wa kijinai,
inayohitaji usiri, hatatoa taarifa yoyote iliyopo kwenye amri hiyo isivyo halali na
makusudi.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni kumi au
kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka mitatu au vyote.
Kuzuia
upelelezi
22. Mtu ambaye kwa makusudi na kinyume cha sheria ataharibu, atafuta,
ataondoa, ataficha, atabadilisha au ataifanya data kompyuta kukosa maana kwa lengo
la kuharibu ushahidi au kuchelewesha upelelezi atakuwa ametenda kosa na akitiwa
hatiani atawajibika kulipa faini ya kiwango kisichopungua milioni tatu au kutumikia
kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja au vyote.
(2) Mtu ambaye kwa makusudi atazuia utekeleza au atashindwa kutekeleza
amri iliyotolewa na sheria hii, atakuwa ametenda kosa na atawajibika, iwapo atatiwa
hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au kutumikia kifungo kwa
kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Unyanyasaji
kwa kupitia
mtandao
23.-(1) Mtu hataanzisha au kukadimisha mawasiliano yoyote ya kielektroniki
kwenda kwa mtu yoyote kwa kutumia mfumo wa kompyuta, kwa lengo la kurubuni,
kulazimisha, kutisha au kunyanyasa au kusababisha maudhi ya hisia.
(2) Mtu akataye kiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
atawajibika, iwapo atatiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua shilingi milioni tatu au
kutumikia kifungo kwa kipindi cha kisichopungua mwaka mmoja au vyote.
Ukiukaji wa
haki bunifu
24.-(1) Mtu hatatumia mfumo wa kompyuta kwa lengo la kukiuka haki bunifu
zinazolindwa na Sheria nyingine yoyote.
(2) Mtu akatayekiuka kifungu kidogo cha (1) atakuwa ametenda kosa na
akitiwa hatiani, atawajibika iwapo ukiukaji (a) hauhusiani na masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyo pungua shilingi
milioni tano au kutumikia kifungo kwa kipindi kisichopungua miaka
mitatu au vyote;
(b) unagusa masuala ya kibiashara, kulipa faini isiyo pungua shilingi milioni
41