Cybercrimes Act
__________________________________________________________________
mtandao au chombo cha kuhifadhia data;
“mtoa njia” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya usambazaji wa data za
kielekroniki kwa kusambaza taarifa zilizotolewa na au kwa mtumiaji wa
huduma katika mtandao wa mawasiliano au anayetoa fursa ya kuingia kwenye
kompyuta au mtandao;
“mhifadhi data ” maana yake ni mtu anayetoa huduma ya uhifadhi wa data za
kielektroniki kwa njia inayojiendesha yenyewe, kwa kupitia mtu kati au kwa
utunzaji wa taarifa kwa muda mfupi kwa madhumuni ya kuwezesha upatikanaji
wa taarifa kwa kwa watumiaji wengine wa huduma kiufanisi zaidi pale
watakapoomba;
“mtoto” maana yake ni mtu mwenye umri chini ya miaka kumi na nane;
“ponografia za watoto” maana yake ni aina yoyote ya picha na filamu za ngono zinazo
ashiria au kumuonesha:
(a) mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi katika matendo ya ngono;
(b) mtu anayeonekana kama mtoto akiwa anashiriki kwa uwazi katika
matendo ya ngono; au
(c) taswira inayoashiria mtoto akiwa anashiriki kwa udhahiri katika matendo
ya ngono;
“mfumo wa kompyuta” maana yake ni kifaa au mchanganyiko wa vifaa, ikijumuisha
mtandao, vifaa vya kuingizia na vya kutolea na ambavyo vinaweza kutumika
pamoja na majalada
yaliyo na programu za kompyuta, maelezo ya
kielektroniki, data za kuingizia na data za kutolea zinazotunza data za hesabu
za miongo zilizo na mantiki na udhibiti wa utolewaji wa mawasiliano na
majukumu mengine;
“data kompyuta” maana yake ni uwasilishaji wa maelezo, dhana, taarifa au maelekezo
katika namna inayofaa kwa ajili ya kuchakata katika
mfumo wa
kompyuta,ikijumuisha programu inayofaa kwa ajili ya kuwezesha mfumo wa
kompyuta kutelekeza kazi fulani;
“chombo cha utunzaji wa data ” maana yake ni kifaa chochote au kitu ambacho
kutoka kwake data kompyuta au taarifa inaweza kuchakata kwenye mfumo wa
kompyuta au kutengenezwa ama kwa msaada wa kifaa kingine au kitu au la;
“kifaa” inajumuisha:
(a) programu ya kompyuta, namba tambuzi, mianzi laini au application;
33